Abstract:
Fikra iliyomo katika mawand̪a ya fasihi ya Kiswahili ni kuwa ut̪end̪i ni maelezo
marefu ya mapisi ya jamii kiushairi. Makala haya yanat̪aka kuonesha kwamba
si t̪end̪i zot̪ʰe zenye madhumuni haya. Kupitiya Ut̪end̪i wa Siri li Asrari
tut̪aonesha kwamba mtʰunzi Mwanalemba alikuwa na niya t̪angu mwanzo ya
kuweka d̪arasa kuhusu hirizi ya majina ya Mwenyezi Mungu. D̪arasa hii
ameigawanya kama namna t̪aasisi za kielimu zinavopendekeza ienreshwe
kiskuli na ameyat̪owa mawazo yake kit̪aalamu. Nadhariya ya Usemezano
kupitiya dhana ya Unrimi imetusaidiya kuuwangaziya ut̪end̪i huu na
tumefaidika na vigezo va: maudhui, ut̪euzi wa misamiat̪i na mitinro ya
uwasilishaji, na mukt̪adha wa matʰumizi ya maneno hayo kama njiya ya
kutambuwa aina ya lugha inayotʰumika. Kwa kwangaziya mitinro ya
uwasilishaji katika d̪arasa ya hirizi tumepata kujuwa kwamba mtʰunzi alikuwa
na dhamira ya kutufunza badala ya kutamba hadithi ya kingano.