University of Kabianga Repository

Kati Ya ‘Choo’ Na ‘Msala’ Ni Neno Lipi Tasfida Imetumika Kimatumizi?

Show simple item record

dc.contributor.author Karama, Mohamed
dc.date.accessioned 2022-09-26T07:12:19Z
dc.date.available 2022-09-26T07:12:19Z
dc.date.issued 2019-10
dc.identifier.uri http://ir-library.kabianga.ac.ke/handle/123456789/412
dc.description.abstract Tasfida ni matumizi ya lugha kwa ustadi unaopunguza makali ya maneno yanayotumiwa. Ikiwa maneno au misemo hiyo ina dalili za kutusi, kukirihi au kuweka maneno mwiko hadharani basi hutumiwa lugha inayoficha sifa hizi mbaya zinazojulikana na jamii. Imejitokeza katika mawanda ya matumizi ya neno ‘choo’ kuwa ni uchafu na hivo wanafunzi wa shule za Msingi na Upili katika mitalaa yao huambiwa wasilitumiye badala yake watumiye ‘msala’ au ‘haja’. Makala haya yameonesha hata hilo neno ‘choo’ piya ni tasfida na lafaa kutumiwa waziwazi katika maongezi ya kawaida. Kufikiya hatuwa hii, tumebainisha matumizi ya maneno ‘choo’, ‘msala’ na ‘haja’ na piya tuliangaziya usuli wa ‘choo’ kiisimu. Uchanganuzi wetu umebaini kuwa neno ‘choo’ latokana na ‘kioo’ lenye maana ya sehemu ya kuoga au kujinadhifisha na hata linapotumiwa kwa maana ya mavi au kinyeshi bado piya ni neno fiche lenye tasfida. Tunahitimisha kuwa kutokana na ‘usafi’ wake, neno ‘choo’ linaweza kutumiwa sawiya na maneno ‘msala’ au ‘haja’ ambayo ni ya mkopo na yenye maana tafauti na kule yalikokopwa. en_US
dc.language.iso other en_US
dc.publisher Himaya ya Kiswahili Tol.1 Chapisho la Chama cha Kiswahili Chuwo Kikuu cha Kabianga (CHAKIKA) en_US
dc.subject Choo en_US
dc.subject Msala en_US
dc.subject Kimatumizi en_US
dc.subject Tasfida en_US
dc.title Kati Ya ‘Choo’ Na ‘Msala’ Ni Neno Lipi Tasfida Imetumika Kimatumizi? en_US
dc.type Article en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Browse

My Account