Abstract:
Shairi la Kutendana katika Sauti ya Dhiki limechanganuliwa, mpaka sasa, kwa
maono ya juujuu kwamba ni shairi la kingono. Kut̪okana na hit̪imisho hili,
Mulokozi amelipuuza kuwa ni shairi lililokosa ubingwa wa kuenreleza
maudhui muhimu yanayotatiza jamii. Makala haya yamebayanisha shairi hili
kuwa ni fumbo la kisiyasa. Kwa kutumiya madhumuni ya ulingamanishaji wa
fasiri ya matukiyo halisi ya kisiyasa katika Kenya wakat̪i huwo na shairi
lenyewe; azimiyo la Abd̪ilat̪if katika shairi lenyewe na namna lilivofikiwa; na
namna azimiyo hilo lilivoathiri msimamo wake wa kisiyasa baad̪a ya kut̪oka
kifungoni, tumeweza kuibuwa maswala muhimu kuhusu maisha ya Abd̪ilat̪if
kabla, wakat̪i wa, na baad̪a ya kut̪oka kifungoni. Nadhariya ya Usemezano
yenye kud̪ulisha maana kut̪okana na usuli, athari, na mwingiliyano wa kauli
nyingi katika mat̪ini na Uhistoriya Mpya yenye kut̪owa fasiri ya matukiyo ya
kihistoriya nrizo nadhariya zilizotumika katika uchanganuzi wetu. Kauli
mbalimbali zilizojit̪okeza katika mashairi kadhaa ya Sauti ya Dhiki na jazanra
zilizotumika zimeweza kufumbuwa ist̪iyara ya shairi hili la Kutendana.
Tumeona wahusika wake (wanawake wawili) wanawakilisha vyama va
kisiyasa va wakat̪i huwo: KANU (KADU), KPU, na Mwanamume
anawakilisha wananchi wa Kenya. Tukiengezeya, Abd̪ilat̪if anajisaili huko
gerezani na kupelekeya afanye azimiyo la kujit̪owa katika siyasa za kijumuiya
sizisothabit̪i na kuwanasihi wasomaji wengine wasiingiye katika mtego aliyouwingiya yeye. Maisha yake ya kisiyasa baad̪a ya kifungo yanaonekana
kufuwata funzo na azimiyo hili.