Abstract:
Fasiri nyengine za kazi za kifasihi zapatikana k̇ a kutiliya maanani
mukṭaďa wa kihistoriya wa kazi hiyo. Fauka ya hayo, iṭikaḍiza kisiyasa,
kiḍini, au kijinsiya ni miyongoni ṁa paradimu zinazoongoza
muwonouliṁengu wa mtunzi wa kazi za kisanaa. Katika mfanyiko huu
wa kučanganya masiyala ya kijamii na ya kiimani nripo uṭafiṭi wetu
ulipoďamiriya kuuhakiki Uṭeṇḍi wa Siri li Asrari uliyotunġa ni
Ṁanaṁarabu binṭi ḂanaLemba mnamo 1662 huko Paṭe, Kenya. Makala
yetu yamejaribu kujibu maswali: mukṭaďa wa kihistoriya wa wakaṭi na
mahali ulimšajiišaje mtunzi kuwasiliša ďamira yake k̇ a mbinu ya
kinahau? Je, ḍini, haswa ďehebu la kiSufi, iličangiyaje
muwonouliṁengu wa mtunzi wakaṭi wa kuwasiliša alama za kiḍini
katika kazi hiyo? Je, suluhišo la mtunzi kuhusu mukṭaďa wa siyasa ya
wakaṭi huwo k̇ a mkonro wa imani yake ulitatuwaje maafa ya wakaṭi
huwo? Tuličanganuwa maṭini ya uṭeṇḍi huu tukiyongozwa ni naďariya
ya uHistoriya Mpya k̇ a k̇ angaziya: alama, jazanra, ṭaswira, siṭiyara,
kiyasi zilivotumiwa na mtunzi na aťari zake katika mfanyiko mzima wa
kisiyasa. Data ya upili ilikusanywa ili tupate fasiri nyenginezo kuṭokana
na mukṭaďa huwo k̇ a sababu hayakujiṭokeza mayelezo haya katika
uṭeṇḍi. Maṭokeyo yetu yanaďihiriša: k̇ a kučanganuliwa luǧa ya nje
kiyasi ya vita va Mtume Muhammaḍ (mhusika nguli) na Anďaruni
(mhusika nruli) ilikuwa ni siṭiyara ya matukiyo ya wakaṭi huwo. Hali
kaďalika, mtunzi ališajiišwa ni matukiyo hayo k̇ enye uwasilišaji wake
ambawo ulifasiri nahau za kusikiya siyasa (hisiya zake za mukṭaďa wa
wakaṭi, mahali, na hali), k̇
ingiliya siyasa (kuyazungumziya matukiyo),
na kuleta siyasa (kukosowa kupita mipaka)—unukuďi wa msimamo wa
aila yake ambao ni sosiyasa (maSufi hawaingii siyasani). Kinyumeče,
data ilipočanganuliwa k̇ a minaṭarafu ya luǧa ya nrani ya kifasihi ya kiSufi iliďihirika maana ya nahau kutumiya siyasa ni kutumiya hekima
kuwaaiďi waumini wamṭegemee Mungu ṭu k̇ a matatuzi ya matatizo
yoṭʰe yanayowakabili hivo “kuvunja upanga” wa siyasa na kuweka
imani k̇ a Ṁenyezi Mungu. Uṭafiṭi wetu una naṭija ya kuwafafanuliya
wanaluǧa umuhimu wa nahau za kiSwahili katika fasihi na haswa ikiwa
nahau hizo zina aťari za uhasi kama lilivo neno siyasa leo.