Kati Ya ‘Choo’ Na ‘Msala’ Ni Neno Lipi Tasfida Imetumika Kimatumizi?

Loading...
Thumbnail Image

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

Himaya ya Kiswahili Tol.1 Chapisho la Chama cha Kiswahili Chuwo Kikuu cha Kabianga (CHAKIKA)

Abstract

Tasfida ni matumizi ya lugha kwa ustadi unaopunguza makali ya maneno yanayotumiwa. Ikiwa maneno au misemo hiyo ina dalili za kutusi, kukirihi au kuweka maneno mwiko hadharani basi hutumiwa lugha inayoficha sifa hizi mbaya zinazojulikana na jamii. Imejitokeza katika mawanda ya matumizi ya neno ‘choo’ kuwa ni uchafu na hivo wanafunzi wa shule za Msingi na Upili katika mitalaa yao huambiwa wasilitumiye badala yake watumiye ‘msala’ au ‘haja’. Makala haya yameonesha hata hilo neno ‘choo’ piya ni tasfida na lafaa kutumiwa waziwazi katika maongezi ya kawaida. Kufikiya hatuwa hii, tumebainisha matumizi ya maneno ‘choo’, ‘msala’ na ‘haja’ na piya tuliangaziya usuli wa ‘choo’ kiisimu. Uchanganuzi wetu umebaini kuwa neno ‘choo’ latokana na ‘kioo’ lenye maana ya sehemu ya kuoga au kujinadhifisha na hata linapotumiwa kwa maana ya mavi au kinyeshi bado piya ni neno fiche lenye tasfida. Tunahitimisha kuwa kutokana na ‘usafi’ wake, neno ‘choo’ linaweza kutumiwa sawiya na maneno ‘msala’ au ‘haja’ ambayo ni ya mkopo na yenye maana tafauti na kule yalikokopwa.

Description

Citation

Endorsement

Review

Supplemented By

Referenced By