University of Kabianga Repository

Uchopekaji wa Vipande vya Simulizi katika Riwaya za S. A. Mohamed, Dunia Yao (2006) na Nyuso na Mwanamke (2010)

Show simple item record

dc.contributor.author Muigai, Mary Njambi
dc.contributor.author Mwamzandi, Issa
dc.contributor.author Oduori, Robert
dc.date.accessioned 2024-08-19T06:55:03Z
dc.date.available 2024-08-19T06:55:03Z
dc.date.issued 2024
dc.identifier.citation Muigai, M. N., Mwamzandi, I., & Oduori, R. (2024). Uchopekaji wa Vipande vya Simulizi katika Riwaya za SA Mohamed, Dunia Yao (2006) na Nyuso na Mwanamke (2010). Journal of Kiswahili and Other African Languages, 2(1), 10-19. en_US
dc.identifier.issn 2958-4914
dc.identifier.uri http://ir-library.kabianga.ac.ke/handle/123456789/867
dc.description Jarida la Uchopekaji wa Vipande vya Simulizi katika Riwaya za S. A. Mohamed, Dunia Yao (2006) na Nyuso na Mwanamke (2010) en_US
dc.description.abstract Makala haya yanachunguza matumizi ya uchopekaji wa vipande vya simulizi katika riwaya mbili za S. A. Mohamed, Dunia Yao (2006) na Nyuso za Mwanamke (2010). Uchunguzi huu uliongozwa na Nadharia ya Ubaadausasa ambayo hupendekeza uanuwai wa mawazo kwa kukaidi kuwepo na mtazamo mmoja wa kueleza ulimwengu na tajriba za binadamu, au simulizi kuu. Uchanganuzi umedhihirisha kuwa mwandishi wa riwaya hizi alitumia kimakusudi vipengele vya kibaadausasa ili kukaidi simulizi kuu zilizotawala. Riwaya hizi zilitumia uchopekaji wa vipande vya simulizi kuvuruga urazini, mshikamano, na muumano wa usimulizi wa riwaya za kimapokeo. Kimaudhui, riwaya hizi zinasaili mwelekeo chanya uliohusishwa na uhuru. Zinaonyesha kuwa mataifa mengi ya Afrika yametawaliwa na hali ya utamauishi baada ya uhuru. Vilevile, misaada inayotolewa na mataifa ya ulaya hutumika kama chambo cha kueneza ukoloni mamboleo katika mataifa ya Afrika. Hali kadhalika, riwaya hizi zinaonyesha changamoto ambazo wahamiaji hupitia wanapohamia ughaibuni kutafuta maisha bora. Ni bayana kuwa mwandishi wa riwaya hizi ametumia mtindo wa uandishi wa ubaadausasa kama mbinu ya kiumbuji inayokaidi uandishi wa kimapokeo. Vilevile, riwaya hizi zimetumika kudhihirisha fujo, ghasia, na ukosefu wa mshikamano katika ulimwengu wa karne ya ishirini na moja. en_US
dc.language.iso en en_US
dc.publisher Journal of Kiswahili and Other African Languages en_US
dc.subject Simulizi kuu en_US
dc.subject Uanuwai en_US
dc.subject Ubaadausasa en_US
dc.subject Uchopekaji en_US
dc.title Uchopekaji wa Vipande vya Simulizi katika Riwaya za S. A. Mohamed, Dunia Yao (2006) na Nyuso na Mwanamke (2010) en_US
dc.type Article en_US


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search DSpace


Browse

My Account