dc.description.abstract |
Lugha ya kimaharajani iliangaziwa mwanzo na Mikhail Bakhtin, mwanaisimu
wa Kirusi na mwitifaki mkuu wa Usemezano. Lugha hii ina sifa za kuweka
kanro kaida za usemaji wa kirasmi na kuwacha wananchi watangamane bila
vizuizi vya kiutawala. Hudhihirisha bezo, ucheshi, upuzi kwa uwazi na kila
mshiriki akafurahiya hali hii. Kulingana na Bakhtin niya haswa ni kupata hisiya
za nrani za watawaliwa, lakini kwa kauli nyengine, watawala huzitumiya fununu
hizi kuzidi kuwatawala wananchi; hichi ndicho kinaya cha umaharajani. Katika
lugha na fasihi ya Kiswahili dhana ya umaharajani bado haijashughulikiwa
ipasavyo seuze maswala ya kidini. Sheikh Juma Amiri ameweza kupata
umaarufu na kuenreleya kualikwa katika hafla mbalimbali Kenya na Afrika
Mashariki kwa sababu ya kuelezeya maswala ya unyumba kwa uwazi
unaoonesha kukiuka kaida za shekhe wa Kiislamu. Makala haya yameonesha
namna Sheikh Juma Amiri anavotumiya maneno, matenro, uigo, sauti, na ishara
za mwili kuelezeya mambo ya unyumba namna yalivozorota, yanavozorotesha
jumuiya ya Waislamu na anapendekeza mbinu mpya wananrowa wazitumiye ili
wafaulishe nrowa zao. Anasuta wanaume, wanawake, mashekhe, wazazi kwa
maneno yaliyojaa jazanra na piya hutumiya maneno yatakayochukuliwa ni
kufuru lau si umaharajani. Anapomaliza darasa zake hadhira inachanganyikiwa
kutojuwa Sheikh Juma Amiri ni nyakanga, kungwi, au ni shekhe? Makala haya
yanahitimisha kuwa kwa kutumiya mbinu hii ya kimaharajani, Sheikh Juma
Amiri amefaulu kufikisha ujumbe wake kiucheshi na kuwateka kimawazo
walengwa watake kumsikiza kila mahali kila wakati. |
en_US |