Ushairi Wa Kezilahabi Ni Ushairi Wa Nabhany: Ushahidi Kutoka Uchanganuzi Wa Umbo La Shairi La Wanajadi

Loading...
Thumbnail Image

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

Jarida la Afrika Mashariki la Masomo ya Kiswahili

Abstract

Makala haya yanakariri hoja kwamba ushairi wa Wagunduzi ni ushairi wa Wanajadi. Mapitiyo yetu ya maandishi yanayozungumziya ushairi wa Kiswahili yameonesha kwamba kuna makundi mawili: Wanajadi, akiwamo Sheikh Nabhany, na Wagunduzi, akiwamo Kezilahabi. Yaliyoandikwa yanaonesha kuwa mgogoro ulizuka kutokana na wanajadi kudai kuwa ushairi wa wagunduzi si wa Kiswahili kwa sababu haufwati urari wa vina na mizani na hivo umbo lake ni tafauti na la mashairi ya Kiswahili. Fauka ya hayo, wachanganuzi wa mashairi ya Kiswahili wana maoni kwamba mashairi ya Kezilahabi ni aina mpya ya mashairi ya Kiswahili. Lengo la makala haya ni kugeuza mwendelezo wa fikira hii. Lengo hili limefikiwa kwa kutumiya uainishaji wa mashairi ya Kiswahili uliyotolewa na Mwanajadi Nabhany kwamba umbo la shairi linatokana na mpangiliyo maalumu wa sauti. Kwa kuchanganuwa umbo la shairi moja la Kezilahabi kupitiya kigezo cha bahari ya utumbuizo, ambayo Nabhany ameiorodhesha kuwa bahari mojawapo ya mashairi ya kijadi ya Kiswahili, tumeona kwamba ushairi wa Kezilahabi una sifa zote, ama karibu zote, za bahari hiyo. Kwa sababu hiyo, tunahitimisha kuwa ushairi wa Kezilahabi ni ushairi wa Wanajadi.

Description

Makala Ya Ushairi Wa Kezilahabi Ni Ushairi Wa Nabhany: Ushahidi Kutoka Uchanganuzi Wa Umbo La Shairi La Wanajadi

Citation

Karama, M., & Mwamzandi, I. (2019). Ushairi wa Kezilahabi ni Ushairi wa Nabhany: Ushahidi Kutoka Uchanganuzi wa Umbo la Shairi la Wanajadi. Jarida la Afrika Mashariki la Masomo ya Kiswahili, 1(1), 7-12.

Endorsement

Review

Supplemented By

Referenced By