Uhalisia mazingaombwe kama mbinu ya mtindo wa uandishi wa ubaadausasa katika riwaya ya Nyuso za Mwanamke (2010) ya S. A. Mohamed

dc.contributor.authorMuigai, Mary Njambi
dc.contributor.authorMwamzandi, Issa Y
dc.contributor.authorOduori, Robert W
dc.date.accessioned2024-09-19T06:58:03Z
dc.date.available2024-09-19T06:58:03Z
dc.date.issued2024-04-24
dc.descriptionJarida la Uhalisia mazingaombwe kama mbinu ya mtindo wa uandishi wa ubaadausasa katika riwaya ya Nyuso za Mwanamke (2010) ya S. A. Mohameden_US
dc.description.abstractMakala haya yamejadili matumizi ya uhalisia mazingaombwe kama mbinu ya mtindo wa uandishi wa ubaadausasa katika riwaya ya Nyuso za Mwanamke (2010) ya S. A. Riwaya hii imedhihirisha upya kwa kukaidi mtindo wa uandishi wa kimapokeo ukiojikita katika uhalisia, na kugeukia mtindo wa uandishi wa kibaadausasa. Makala haya yanachunguza matumizi ya uhalisia mazingaombwe katika riwaya hii, kama kipengele mojawapo cha mtindo wa uandishi wa ubaadausasa. Lengo kuu la makala haya ni kubainisha vipengele vya uhalisia mazingaombwe na namna vimetumika katika riwaya ya Nyuso za Mwanamke. Makala haya yameongozwa na Nadharia ya Ubaadausasa inayopendekeza uanuwai wa mawazo kwa kukaidi kuwepo na mtazamo mmoja wa kueleza tajriba tofauti za binadamu, au simulizi kuu. Sampuli dhamirifu ilitumika kuteua riwaya ya hii. Data ilipatikana kupitia usomaji wa kina wa riwaya. Data ilichanganuliwa kwa kuzingatia mihimili ya Nadharia ya Ubaadausasa na kuwasilishwa kwa maelezo ya kinathari. Matokeo yalibainisha kwamba riwaya hii iliziba mipaka kati ya uhalisia na umazingaombwe kupitia matumizi ya wahusika binadamu wenye nguvu za ajabu kama vile kuwasoma watu. Aidha, riwaya hii ilitumia viumbe wa ajabu kama vile mizuka, vivuli, majini na wafu kuwakilisha hali halisi ya dunia ya sasa ambayo imejaa mambo mengi ya ajabu yasiyoelezeka. Katika kutamatisha, ilibainika kuwa matumizi ya uhalisia mazingaombwe ni mbinu ya kiumbuji anayotumiwa mwandishi kukaidi simulizi kuu ya uandishi wa kimapokeo wa riwaya ya Kiswahili uliojikita katika uhalisia. Matumizi ya mtindo huu ni dhihirisho la mabadiliko katika uandishi wa riwaya ya Kiswahili.en_US
dc.identifier.citationMuigai, M. N., Mwamzandi, I. Y., & Oduori, R. W. (2024). Uhalisia mazingaombwe kama mbinu ya mtindo wa uandishi wa ubaadausasa katika riwaya ya Nyuso za Mwanamke (2010) ya S. A. Mohamed. Editon consortium journal of Kiswahili, 5(1), 11-20. https://doi.org/10.51317/ecjkisw.v5i1.480en_US
dc.identifier.issn2663 - 9289
dc.identifier.urihttp://ir-library.kabianga.ac.ke/handle/123456789/879
dc.language.isootheren_US
dc.publisherEditon Consortium Journal of Kiswahilien_US
dc.subjectSimulizi kuuen_US
dc.subjectUbaadausasaen_US
dc.subjectUhalisiaen_US
dc.subjectUhalisia mazingaombween_US
dc.titleUhalisia mazingaombwe kama mbinu ya mtindo wa uandishi wa ubaadausasa katika riwaya ya Nyuso za Mwanamke (2010) ya S. A. Mohameden_US
dc.typeArticleen_US

Files

Original bundle

Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Mary+Njambi+Muigai_Vol.5.+Issue+1.+ECJK.+April+2024..pdf
Size:
608.25 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Research Article

License bundle

Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: