Uhalisia mazingaombwe kama mbinu ya mtindo wa uandishi wa ubaadausasa katika riwaya ya Nyuso za Mwanamke (2010) ya S. A. Mohamed

Loading...
Thumbnail Image

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

Editon Consortium Journal of Kiswahili

Abstract

Makala haya yamejadili matumizi ya uhalisia mazingaombwe kama mbinu ya mtindo wa uandishi wa ubaadausasa katika riwaya ya Nyuso za Mwanamke (2010) ya S. A. Riwaya hii imedhihirisha upya kwa kukaidi mtindo wa uandishi wa kimapokeo ukiojikita katika uhalisia, na kugeukia mtindo wa uandishi wa kibaadausasa. Makala haya yanachunguza matumizi ya uhalisia mazingaombwe katika riwaya hii, kama kipengele mojawapo cha mtindo wa uandishi wa ubaadausasa. Lengo kuu la makala haya ni kubainisha vipengele vya uhalisia mazingaombwe na namna vimetumika katika riwaya ya Nyuso za Mwanamke. Makala haya yameongozwa na Nadharia ya Ubaadausasa inayopendekeza uanuwai wa mawazo kwa kukaidi kuwepo na mtazamo mmoja wa kueleza tajriba tofauti za binadamu, au simulizi kuu. Sampuli dhamirifu ilitumika kuteua riwaya ya hii. Data ilipatikana kupitia usomaji wa kina wa riwaya. Data ilichanganuliwa kwa kuzingatia mihimili ya Nadharia ya Ubaadausasa na kuwasilishwa kwa maelezo ya kinathari. Matokeo yalibainisha kwamba riwaya hii iliziba mipaka kati ya uhalisia na umazingaombwe kupitia matumizi ya wahusika binadamu wenye nguvu za ajabu kama vile kuwasoma watu. Aidha, riwaya hii ilitumia viumbe wa ajabu kama vile mizuka, vivuli, majini na wafu kuwakilisha hali halisi ya dunia ya sasa ambayo imejaa mambo mengi ya ajabu yasiyoelezeka. Katika kutamatisha, ilibainika kuwa matumizi ya uhalisia mazingaombwe ni mbinu ya kiumbuji anayotumiwa mwandishi kukaidi simulizi kuu ya uandishi wa kimapokeo wa riwaya ya Kiswahili uliojikita katika uhalisia. Matumizi ya mtindo huu ni dhihirisho la mabadiliko katika uandishi wa riwaya ya Kiswahili.

Description

Jarida la Uhalisia mazingaombwe kama mbinu ya mtindo wa uandishi wa ubaadausasa katika riwaya ya Nyuso za Mwanamke (2010) ya S. A. Mohamed

Citation

Muigai, M. N., Mwamzandi, I. Y., & Oduori, R. W. (2024). Uhalisia mazingaombwe kama mbinu ya mtindo wa uandishi wa ubaadausasa katika riwaya ya Nyuso za Mwanamke (2010) ya S. A. Mohamed. Editon consortium journal of Kiswahili, 5(1), 11-20. https://doi.org/10.51317/ecjkisw.v5i1.480

Endorsement

Review

Supplemented By

Referenced By