Mchakato wa Uandishi Bunifu kama Unavyoakisiwa katika Riwaya za Kisasa za K.W. Wamitila

dc.contributor.authorJanice M. Mutua
dc.contributor.authorIssa Mwamzandi
dc.contributor.authorAbdulRahim Taib
dc.date.accessioned2026-06-10T08:23:07Z
dc.date.issued2021
dc.description.abstractMakala hayaimejibana katika ufafanuzi wa upekee wa mtunzi wa riwaya za Kiswahili za kisasa pamoja na changamoto anazopitia mikononi mwa wahariri na wachapishaji kama inavyopendekezwa katika riwaya zenyewe. Aidha, makala imependekeza njia za kuboresha na kukuza riwaya mpya za Kiswahili. Madhumuni yake ni kufafanua mchakato mzima wa uandishi wa riwaya mpya kwa kuwaangazia wahusika watatu muhimu yaani mwandishi, msomaji na mchapishaji. Nadharia ya usasaleo imeuongoza mjadala huu katika ukusanyaji na uchanganuzi wa data. Mintarafu ya nadharia, mtunzi wa kazi bunifu ana uhuru wa kuandika jinsi apendavyo, hailazimu kwamba riwaya zifuate utaratibu mahususi. Mkabala wa uchanganuzi wa yaliyomo ulitumika kuchanganua data iliyohusiana na swala zima la ubunifu na uchapishaji wa riwaya mpya ya Kiswahili. Data ilichanganuliwa kwa kuangazia maudhui na vipengele vya mbinu za kimajaribio kama vile dayolojia, urejeleomatini, simulizi fupi na taashira. Riwaya za Mwandishi, Msomaji na Mchapishajii na Musaleo! zimetumika kuangazia mchakato huu. Matokeo yamewasilishwa kwa njia ya maelezo. Imebainika kuwa sura na ubunifu wa riwaya mpya ni zao la usomi. Ili kuelewa ujumbe katika riwaya za kisasa ni muhimu kwa ‘mhariri’ kufanya utafiti wa kina kabla ya kutoa mapendekezo yake kwa mchapishaji. Aidha, inailazimu hadhira kuwa na ufahamu wa mambo mengi kiada ili kung’amua yanayowasilishwa katika riwaya za kisasa.
dc.identifier.citationMutua, J. M., Mwamzandi, I., & Taib, A. (2021). Mchakato wa Uandishi Bunifu kama Unavyoakisiwa katika Riwaya za Kisasa za KW Wamitila. Mwanga wa Lugha, 6(2), 15-26.
dc.identifier.urihttps://ir-library.kabianga.ac.ke/handle/123456789/1202
dc.language.isoother
dc.publisherMwanga wa Lugha, 6(2), 15-26.
dc.subjectKariha
dc.subjectRiwaya za Kisasa
dc.subjectMwandishi
dc.subjectUandishi bunifu
dc.subjectMhariri
dc.subjectMchapishaji.
dc.titleMchakato wa Uandishi Bunifu kama Unavyoakisiwa katika Riwaya za Kisasa za K.W. Wamitila
dc.typeArticle

Files

Original bundle

Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Jarida+la+Mwanga_6(2)_15-26.pdf
Size:
511.87 KB
Format:
Adobe Portable Document Format

License bundle

Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: