Mchakato wa Uandishi Bunifu kama Unavyoakisiwa katika Riwaya za Kisasa za K.W. Wamitila
Loading...
Date
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Mwanga wa Lugha, 6(2), 15-26.
Abstract
Makala hayaimejibana katika ufafanuzi wa upekee wa mtunzi wa riwaya za Kiswahili za
kisasa pamoja na changamoto anazopitia mikononi mwa wahariri na wachapishaji kama
inavyopendekezwa katika riwaya zenyewe. Aidha, makala imependekeza njia za
kuboresha na kukuza riwaya mpya za Kiswahili. Madhumuni yake ni kufafanua
mchakato mzima wa uandishi wa riwaya mpya kwa kuwaangazia wahusika watatu
muhimu yaani mwandishi, msomaji na mchapishaji. Nadharia ya usasaleo imeuongoza
mjadala huu katika ukusanyaji na uchanganuzi wa data. Mintarafu ya nadharia, mtunzi
wa kazi bunifu ana uhuru wa kuandika jinsi apendavyo, hailazimu kwamba riwaya
zifuate utaratibu mahususi. Mkabala wa uchanganuzi wa yaliyomo ulitumika
kuchanganua data iliyohusiana na swala zima la ubunifu na uchapishaji wa riwaya mpya
ya Kiswahili. Data ilichanganuliwa kwa kuangazia maudhui na vipengele vya mbinu za
kimajaribio kama vile dayolojia, urejeleomatini, simulizi fupi na taashira. Riwaya
za Mwandishi, Msomaji na Mchapishajii na Musaleo! zimetumika kuangazia mchakato
huu. Matokeo yamewasilishwa kwa njia ya maelezo. Imebainika kuwa sura na ubunifu
wa riwaya mpya ni zao la usomi. Ili kuelewa ujumbe katika riwaya za kisasa ni muhimu
kwa ‘mhariri’ kufanya utafiti wa kina kabla ya kutoa mapendekezo yake kwa
mchapishaji. Aidha, inailazimu hadhira kuwa na ufahamu wa mambo mengi kiada ili
kung’amua yanayowasilishwa katika riwaya za kisasa.
Description
Keywords
Citation
Mutua, J. M., Mwamzandi, I., & Taib, A. (2021). Mchakato wa Uandishi Bunifu kama Unavyoakisiwa katika Riwaya za Kisasa za KW Wamitila. Mwanga wa Lugha, 6(2), 15-26.
