Mitazamo ya Kiskaz Kuhusu Covid-19 Inavyojitokeza katika Lugha ya Wananchi Nchini Kenya

dc.contributor.authorRotich, Alexander
dc.date.accessioned2024-02-27T09:53:13Z
dc.date.available2024-02-27T09:53:13Z
dc.date.issued2024
dc.descriptionJarida la Mitazamo ya Kiskaz Kuhusu Covid-19 Inavyojitokeza katika Lugha ya Wananchi Nchini Kenyaen_US
dc.description.abstractMadhumni ya makala haya yalikuwa ni kubainisha na kuchanganua mitazamo ya WaKenya kuhusu Tangaavu la Korona (COVID-19) kama inavyodhihirika kupitia mazungumzo ya kikawaida, Skaz. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, tafiti za awali kuhusu mada hii hazikukitwa katika misingi ya Skaz. Kwa hivyo, taarifa nyingi kuhusu Tangaavu la Korona zilizowasilishwa na Shirika la Afya Ulimwenguni pamoja na Wizara ya Afya nchini Kenya zilikuwa za kitaalamu (kiakademia). Utafiti huu ulikuwa wa nyanjani na ulifanyika Kericho, Kenya. Mtafiti aliteua sampuli kimakusudi na kukusanya data kwa kutumia mbinu ya utazamaji nyanjani. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni ya Usemezano ikijumuisha sifa za Skaz kama ilivyoelezwa na Bakhtin ikitiliwa nguvu na Mbinu ya Urazini wa Kiwatu kama ilivyoendelezwa na Sacks na wenzake. Uchanganuzi wa data ulionesha kuwa, mwanzomwanzo, kutokana na kukosa ufahamu wa kitaaluma kuhusu ugonjwa “mpya” Tangaavu la COVID-19 kwa jumla, bila kukusudia kupotosha WaKenya waliibuka na mitazamo mbalimbali kuhusu ugonjwa huu. Mitazamo hii pia ilitokana na jitihada za hekaheka kutafuta njia za kuzuia usambazaji na hata tiba miongoni mwa wanajamii. Utafiti huu umeweka wazi mitazamo “hasi” kuhusu ugonjwa wa COVID-19 jinsi ili(na)vyodhihirika katika mazungumzo ya kikawaida na hivyo kuwafaidi watafiti wa utabibu na wapangaji sera za kiserikali kutilia maanani mitazamo katika lugha ya kikawaida haswa kwenye majanga ya kiulimwengu.en_US
dc.identifier.citationRotich, A. (2024). Mitazamo ya Kiskaz Kuhusu Covid-19 Inavyojitokeza katika Lugha ya Wananchi Nchini Kenya. East African Journal of Swahili Studies, 7(1), 79-86. https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1754.en_US
dc.identifier.uri: https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1754
dc.identifier.urihttp://ir-library.kabianga.ac.ke/handle/123456789/756
dc.language.isootheren_US
dc.publisherEast African Journal of Swahili Studiesen_US
dc.subjectSkazen_US
dc.subjectCOVID-19en_US
dc.subjectMtazamoen_US
dc.subjectKizuizuien_US
dc.subjectKerichoen_US
dc.titleMitazamo ya Kiskaz Kuhusu Covid-19 Inavyojitokeza katika Lugha ya Wananchi Nchini Kenyaen_US
dc.typeArticleen_US

Files

Original bundle

Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Alexander.pdf
Size:
271.55 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Original Research

License bundle

Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: