Mitazamo ya Kiskaz Kuhusu Covid-19 Inavyojitokeza katika Lugha ya Wananchi Nchini Kenya

Loading...
Thumbnail Image

Date

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

East African Journal of Swahili Studies

Abstract

Madhumni ya makala haya yalikuwa ni kubainisha na kuchanganua mitazamo ya WaKenya kuhusu Tangaavu la Korona (COVID-19) kama inavyodhihirika kupitia mazungumzo ya kikawaida, Skaz. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, tafiti za awali kuhusu mada hii hazikukitwa katika misingi ya Skaz. Kwa hivyo, taarifa nyingi kuhusu Tangaavu la Korona zilizowasilishwa na Shirika la Afya Ulimwenguni pamoja na Wizara ya Afya nchini Kenya zilikuwa za kitaalamu (kiakademia). Utafiti huu ulikuwa wa nyanjani na ulifanyika Kericho, Kenya. Mtafiti aliteua sampuli kimakusudi na kukusanya data kwa kutumia mbinu ya utazamaji nyanjani. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni ya Usemezano ikijumuisha sifa za Skaz kama ilivyoelezwa na Bakhtin ikitiliwa nguvu na Mbinu ya Urazini wa Kiwatu kama ilivyoendelezwa na Sacks na wenzake. Uchanganuzi wa data ulionesha kuwa, mwanzomwanzo, kutokana na kukosa ufahamu wa kitaaluma kuhusu ugonjwa “mpya” Tangaavu la COVID-19 kwa jumla, bila kukusudia kupotosha WaKenya waliibuka na mitazamo mbalimbali kuhusu ugonjwa huu. Mitazamo hii pia ilitokana na jitihada za hekaheka kutafuta njia za kuzuia usambazaji na hata tiba miongoni mwa wanajamii. Utafiti huu umeweka wazi mitazamo “hasi” kuhusu ugonjwa wa COVID-19 jinsi ili(na)vyodhihirika katika mazungumzo ya kikawaida na hivyo kuwafaidi watafiti wa utabibu na wapangaji sera za kiserikali kutilia maanani mitazamo katika lugha ya kikawaida haswa kwenye majanga ya kiulimwengu.

Description

Jarida la Mitazamo ya Kiskaz Kuhusu Covid-19 Inavyojitokeza katika Lugha ya Wananchi Nchini Kenya

Citation

Rotich, A. (2024). Mitazamo ya Kiskaz Kuhusu Covid-19 Inavyojitokeza katika Lugha ya Wananchi Nchini Kenya. East African Journal of Swahili Studies, 7(1), 79-86. https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.1754.

Endorsement

Review

Supplemented By

Referenced By