Vipengele vya uwasilishaji wa wahusika wa kimazingaombwe na uhusika: Mifano katika Watu wa Gehenna na Babu Alipofufuka

Loading...
Thumbnail Image

Date

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

Jarida la Afrika Mashariki la masomo ya Kiswahili,

Abstract

Makala haya yanatathmini uwasilishaji wa wahusika wa kimazingaombwe na uhusika katika kazi za Kiswahili. Uchanganuzi huu ni wa kimaktaba tukizingatia mihimili ya nadharia ya Umazingaombwe. Riwaya za Babu Alipofufuka na Watu wa Gehenna zilichaguliwa kimakusudi kwa sababu uwasilishaji umechochewa na mbinu ajabuajabu za waandishi katika uhusika na usawirishaji wa wahusika kwa njia unaojenga dhamira ya kimazingaombwe. Uwasilishaji huu unazua utata kwa wasomaji katika kunata ujumbe unaowasilishwa na wahusika hao katika riwaya hizi teule za kimajaribio. Waandishi hawa, Wamitia na Olali, wanasukanisha uhalisia uliochongwa kwa njia maalum katika ruwaza inayobadilikabadilika daima, huku wakiwakilisha matukio ya kawaida na maelezo ya kina sambamba na vipengee vya kifantasia na kindoto na kwa kutumia mambo yaliyotokana na visasili na hekaya. Aidha, kazi hii ilidhamiria kuthibitisha uwasilishaji wa kiuhalisajabu katika mandari au mazingira ya kimazingaombwe. Utafiti huu umejaribu kujaliza mapengo yanayoleta matatizo ya ufahamu na usadikifu wa kazi tulizo teua za kihalisiajabu. Maandishi katika utafiti huu yanadhamiria kukuza na kupanua uelewekaji wa riwaya za kisasa mbali na kufaidi wasomaji mbalimbali na hata kuwapa motisha wahakiki kushughulikia zaidi wahusika, uhusika na uwasilishaji katika misingi ya umazingaombwe katika fasihi simulizi.

Description

Uwasilishaji wa wahusika wa kimazingaombwe na uhusika

Citation

Kenduiywa, A. C., Mwamzandi, I., & Kisurulia, S. (2020). Vipengele vya Uwasilishaji wa Wahusika wa Kimazingaombwe na Uhusika: Mifano katika Watu wa Gehenna na Babu Alipofufuka. Jarida la Afrika Mashariki la Masomo ya Kiswahili, 2(1), 1-7.

Endorsement

Review

Supplemented By

Referenced By