Darasa Za Kimaharajani Za Nyakanga-Kungwi-Sheikh Juma Amiri Kuhusu Unyumba

dc.contributor.authorKarama, Mohamed
dc.date.accessioned2022-09-30T10:35:08Z
dc.date.available2022-09-30T10:35:08Z
dc.date.issued2019
dc.descriptionJarida la Darasa Za Kimaharajani Za Nyakanga-Kungwi-Sheikh Juma Amiri Kuhusu Unyumbaen_US
dc.description.abstractLugha ya kimaharajani iliangaziwa mwanzo na Mikhail Bakhtin, mwanaisimu wa Kirusi na mwitifaki mkuu wa Usemezano. Lugha hii ina sifa za kuweka kanro kaida za usemaji wa kirasmi na kuwacha wananchi watangamane bila vizuizi vya kiutawala. Hudhihirisha bezo, ucheshi, upuzi kwa uwazi na kila mshiriki akafurahiya hali hii. Kulingana na Bakhtin niya haswa ni kupata hisiya za nrani za watawaliwa, lakini kwa kauli nyengine, watawala huzitumiya fununu hizi kuzidi kuwatawala wananchi; hichi ndicho kinaya cha umaharajani. Katika lugha na fasihi ya Kiswahili dhana ya umaharajani bado haijashughulikiwa ipasavyo seuze maswala ya kidini. Sheikh Juma Amiri ameweza kupata umaarufu na kuenreleya kualikwa katika hafla mbalimbali Kenya na Afrika Mashariki kwa sababu ya kuelezeya maswala ya unyumba kwa uwazi unaoonesha kukiuka kaida za shekhe wa Kiislamu. Makala haya yameonesha namna Sheikh Juma Amiri anavotumiya maneno, matenro, uigo, sauti, na ishara za mwili kuelezeya mambo ya unyumba namna yalivozorota, yanavozorotesha jumuiya ya Waislamu na anapendekeza mbinu mpya wananrowa wazitumiye ili wafaulishe nrowa zao. Anasuta wanaume, wanawake, mashekhe, wazazi kwa maneno yaliyojaa jazanra na piya hutumiya maneno yatakayochukuliwa ni kufuru lau si umaharajani. Anapomaliza darasa zake hadhira inachanganyikiwa kutojuwa Sheikh Juma Amiri ni nyakanga, kungwi, au ni shekhe? Makala haya yanahitimisha kuwa kwa kutumiya mbinu hii ya kimaharajani, Sheikh Juma Amiri amefaulu kufikisha ujumbe wake kiucheshi na kuwateka kimawazo walengwa watake kumsikiza kila mahali kila wakati.en_US
dc.identifier.citationKarama, M. (2019). Darasa za Kimaharajani za Nyakanga-Kungwi-Sheikh Juma Amiri Kuhusu Unyumba. Jarida la Afrika Mashariki la Masomo ya Kiswahili, 1(4), 129-141.en_US
dc.identifier.issn1476-4687
dc.identifier.urihttp://ir-library.kabianga.ac.ke/handle/123456789/416
dc.language.isootheren_US
dc.publisherJarida la Afrika Mashariki la Masomo ya Kiswahilien_US
dc.subjectUsemezanoen_US
dc.subjectUnyumbaen_US
dc.subjectMaharajanien_US
dc.titleDarasa Za Kimaharajani Za Nyakanga-Kungwi-Sheikh Juma Amiri Kuhusu Unyumbaen_US
dc.typeArticleen_US

Files

Original bundle

Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
DARASA ZA.pdf
Size:
287.54 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Full article

License bundle

Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: