Ushairi Wa Kisufi Katika Tendi Za Kale Za Kiswahili: Mfano Wa Utendi Wa Siri Li Asrari

Loading...
Thumbnail Image

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

The Africa Premier Research Publishing Hub

Abstract

Usufi ni njia mojawapo ya kumuabudu Mungu katika dini ya Kiislamu. Kuna tariqa kadhaa za kisufi katika Afrika Mashariki na zote zina lengo moja kuu la kumpwekesha Mungu. Nyingi ya tendi za kale za Kiswahili, haswa za kabla ya Karne ya Ishirini, zina maudhui kuhusu dini ya Kiislamu. Makala haya yanaangaza kuhusu njia hii ya kumpwekesha Mungu kwa kutumia ushairi wa tendi ili kufikiliza ujumbe huu wa kisufi. Nadharia ya Usemezano inashikilia kwamba maana haswa ya neno hupatikana kwa kuangalia muktadha wa maneno yalipo(vyo)tumika katika kauli nzima. Kwa kutumia msingi huu wa kuchunguza muktadha tutathibitisha kauli yetu kwamba tendi za kale za Kiswahili zina athari ya kisufi na katika Utendi wa Siri li Asrari ndipo tutakapochukua data yetu. Tumesampulisha itikadi, daraja, na lugha ya kisufi inavyojidhihirisha kwenye utendi huu na kutoa uchanganuzi wa kimaelezo. Tunahitimisha kwamba usufi umemwathiri kwa kiwango kikubwa mtunzi wa utendi huu na lengo lake na la kisufi ni moja – kumpwekesha Mungu

Description

Jarida la Ushairi Wa Kisufi Katika Tendi Za Kale Za Kiswahili: Mfano Wa Utendi Wa Siri Li Asrari

Citation

Endorsement

Review

Supplemented By

Referenced By