Usemezano katika nyimbo za amani miongoni mwa jamii tatu teule za Kenya

Loading...
Thumbnail Image

Date

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

Jarida la Afrika mashariki la masomo ya Kiswahil

Abstract

Utafiti huu ulichunguza usemezano katika nyimbo za amani za jamii tatu za Kenya. Nyimbo zilizoshughulikiwa ni zile zilizoimbwa baada ya ghasia zilizoshuhudiwa nchini Kenya baada ya uchaguzi wa kitaifa uliofanywa mwaka wa 2007. Kazi hii ilichochewa na uharibifu mkubwa wa mali na vifo vya watu usioweza kumithilika hasa kwa vile nchi ya Kenya ilikuwa haijawahi kuipitia hali kama hiyo wakati mwingine. Azma kuu ya utafiti huu ilikuwa kubainisha sifa za usemezano katika nyimbo za amani miongoni mwa jamii za Wakipsigis, Wakisii na Waluo. Kwa kufanya hivyo, uchunguzi huu ulilenga kuchunguza athari za mazingira na muktadha wa kijamii katika utunzi na uimbaji wa nyimbo za amani. Aidha, kazi hii ilidhamiria kufafanua dhana ya shani kama inavyojitokeza katika nyimbo za amani. Hali kadhalika, kazi hii ilibainisha nyimbo kama kauli ambazo hujibu na kutarajia majibu kuhusu amani. Utafiti huu ulishughulikia jumla ya nyimbo ishirini zenye maudhui ya kukuza amani na maridhiano kutoka jamii tatu za Kenya zilizoathirika katika ghasia zilizozuka baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa. Jamii zenyewe ni Wakipsigis, Wakisii na Waluo. Utafiti huu uliendelezwa katika Kaunti za Kericho, Bomet, Nyamira na Nyando na ulishirikisha nyimbo zilizoimbwa baina ya mwaka wa 2008 na 2013. Nyimbo tano kutoka kila jamii husika ziliteuliwa kimakusudi na kisha kuhakikiwa. Nyimbo nyingine tano zilizoimbwa kwa lugha ya Kiswahili kutoka jamii tatu teule katika uchunguzi huu zilishughulikiwa pia katika kazi hii. Nyimbo za wanamuziki kutoka jamii zilizohusishwa zilikusanywa na kuhakikiwa. Kwa hivyo, data za kimsingi zilitokana na nyimbo zilizorekodiwa kwenye sidii. Aidha, uchunguzi maktabani uliendelezwa kwa kurejelea kazi mbalimbali za awali zilizowahi kushughulikiwa kuhusu nyimbo. Habari nyingine zilikusanywa katika mtandao. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya usemezano iliyoasisiwa na Mikhail Bakhtin. Uchanganuzi wa kimaelezo ulitumiwa katika kuchanganua data. Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kuwa nyimbo huwa na uwezo mkubwa wa kuielekeza jamii kwa njia mbalimbali. Kwa sababu hii, jamii hupokea ushauri na maelekezo juu ya umuhimu wa kukuza utangamano, amani na maridhiano kupitia nyimbo. Aidha, nyimbo huweza kutumiwa kama njia mojawapo ya kuiponya jamii pindi inapokumbwa na hali tata iletwayo na michafuko.

Description

Tasnifu hii imetolewa ili kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili wa sanaa katika Kiswahili katika chuo kikuu cha Kabianga

Citation

Kurgat, E., & Mwamzandi, I. (2019). Usemezano Katika Nyimbo za Amani: Athari za Muktadha wa Kijamii Katika Utunzi na Uimbaji wa Nyimbo za Mhubiri Joel Kimetto na Mwinjilisti Philip Rono. Jarida la Afrika Mashariki la Masomo ya Kiswahili, 1(3), 118-128.

Endorsement

Review

Supplemented By

Referenced By