Hongera Ni Ungonočoro; Ifikiriwe Ṭena Maana Yake K̇enye Makamusi Ya Kileo

Loading...
Thumbnail Image

Date

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

East African Journal of Swahili Studies

Abstract

Mabaḍiliko ya kisemantiki ni haliya isiyopingika katika ukuwaji wa luǧa yoyoṭʰe ulimwenguni. Pahala pamoja ambapo maneno huhifaďiwa k̇ a matumiyaji ya sasa na ya vizazi vijavo ni makamusini. Makamusi hukusanya maana za mingi ya maneno yanayotumika katika jamii na k̇ amo mabaḍiliko ya kisemantiki hujiṭokeza. Makala haya yamelenga kuṭaťmini maana ya neno “hongera” k̇ enye makamusi ya kiSwahili ya awali na ya kileo minṭarafu ya uṭamaḍuni wa waSwahili, wekahazina wa luǧa ya kiSwahili. Maďumuni ya uṭafiṭi wetu yalikuwa kučanganuwa maana ya neno hongera kama msamiyaṭi k̇ enye makamusi; kučunguza maana ya neno hongera katika mila za waSwahili; na kuṭaťmini uwafiki wa matumiyaji mapana ya neno hongera katika jamii leo. Naďariya ya Usemezano, iliyoongoza uṭafiṭi huu, inafafanuwa kuwa maana haswa ya neno hupatikana k̇ a k̇ angaliya vigezo va usuli, mapisi, mukṭaďa, sajili, uṭamaḍuni, ainaṭi za luǧa zilizomo k̇ enye lugha hiyo; la sivo, tuṭapata maana ya kijuujuu au ya kikamusi. Data yetu tuliikusanya k̇ a kuwauliza, kupitiya mahojiyano yasomuunro, wasailiwa 5 wa marika zetu (wa miyaka 55 k̇ enra chini) na piya wazee 5 (wa miyaka 70 na zaiḍi) kuhusu usuli, mukṭaďa wa matumiyaji, na mafafanuzi ya kiṭamaḍuni juu ya neno hilo “hongera”. Aiďan maaṇḍiko ya waṭaalamu na makamusi yenye ťika piya yalipitiwa na kučanganuliwa ili kutupa data ya neno “hongera”; kupunguza mlemeyo wowoṭʰe wa wahijowa; na piya kuhakikiša mayelezo ya wasailiwa. Uṭafiṭi wetu uliťibiṭiša kuwa hongera latumika k̇ a maana ya “kupongeza” ṭu k̇ enye makamusi ṭajika ya kiSwahili sanifu ya kileo, k̇ a mfano, Kamusi Kuu ya Kiswahili (2016). Awali, katika makamusi asasi ya Krapf (1882) na Sacleux (1891/1939), maana ya hongera imeťubuṭu kumaaniša awamu katika šerehe ya ṭohara au ni kufariji k̇ a mikasa iliyompata mtʰu. Aiďan, maṭokeyo yetu yaligunruwa kuwa “hongera” ni neno limaanišalo “pʰole” katika kiSwahili Asiliya (lahaja za ṗani Afrika Mašariki) lakini maana hii imevunjwa na maana ya kiṭamaḍuni k̇ a sababu ni awamu katika šerehe ya ṭohara, piya ni awamu katika šerehe ya harusi ya kiSwahili haswahaswa wakati wa ḃanaharusi k̇ ingiya nrani kuwonana na biharusi kimwili. Kimila ya waSwahili neno hili ni ṁiko wa daraja ya juu—lahusu ngono—hivo hwanika ungonočoro linapotumika pasipo. Lengo la uṭafiṭi huu ni kušauri ifikiriwe ṭena maana ya neno hongera katika makamusi ya kileo. Uṭafiṭi huu una naṭija k̇ a wanaleksikografiya kufanya uṭafiṭi zaiḍi wanapotengeza makamusi. Piya uṭawafaa wanaiḍara ya uṭamaḍuni katika mamlaka kujuwa asili na mila za watumiyaji wa luǧa hii ya kiSwahili na nyenginezo ṇčini.

Description

Citation

Karama, M. (2024). Hongera Ni Ungonočoro; Ifikiriwe Ṭena Maana Yake K̇ enye Makamusi Ya Kileo. East African Journal of Swahili Studies, 7(1), 416-428. https://doi.org/10.37284/jammk.7.1.2258.

Endorsement

Review

Supplemented By

Referenced By