Changamoto Zinazokabili Umiliki na Matumizi ya Ardhi Barani Afrika: Udurusu wa Riwaya Tatu za Karne ya 21

dc.contributor.authorArthur K. Muhia
dc.contributor.authorIssa Y. Mwamzandi
dc.date.accessioned2026-06-10T08:12:20Z
dc.date.issued2022
dc.description.abstractMakala haya yanachanganua suala la changamoto zinazokabili umiliki na matumizi ya ardhi barani Afrika kama lilivyosawiriwa katika riwaya za karne ya ishirini na moja, kwa kurejelea riwaya za Chozi la Heri (2014), Msimu wa Vipepeo (2009) na Nakuruto (2006). Ardhi ni miongoni mwa rasilimali muhimu katika maisha ya binadamu hasa katika uzalishaji mali. Huwa chanzo cha mahitaji ya kimsingi kama vile chakula na makaazi. Aidha, uwezo wa kumiliki ardhi huwa ni sifa kuu ya maendeleo na mabadiliko mengi katika jamii ambayo yamewahi kushuhudiwa duniani. Tungo za kifasihi tulizoziteua kimakusudi zilifanikisha utafiti huu kwa sababu fasihi huwa imefungamanishwa kibunifu na maisha halisi ya binadamu. Sifa kuu ya riwaya hizi ni kwamba zimeliangazia suala la ardhi kwa mapana. Isitoshe, zimetungwa katika kipindi cha karne ya ishirini na moja ambacho utandawazi umeenea na kuimarika barani Afrika. Ili kufanikisha udurusu huu, tuliligawa suala letu la utafiti katika sehemu tatu kuu: kipindi cha kabla ya ukoloni, kipindi cha ukoloni na kipindi cha utandawazi. Uchanganuzi matini huu wa kimaktaba uliongozwa na nadharia ya Baada-ukoloni. Umuhimu wa makala haya unatarajiwa kuwa pamoja na kudhihirisha mitazamo ya watunzi mbalimbali kuhusu changamoto katika umiliki na matumizi ya ardhi barani Afrika; pamoja na mapendekezo ya namna za kuzitatua. Tunatarajia kutoa mchango wa kitaaluma kuhusiana na suala hili hivyo kuwafaa watafiti wa baadaye na watunga sera zinazohusiana na suala la umiliki na matumizi ya ardhi barani Afrika.
dc.identifier.citationMuhia, A. K., & Mwamzandi, I. Y. (2022). Changamoto Zinazokabili Umiliki na Matumizi ya Ardhi Barani Afrika: Udurusu wa Riwaya Tatu za Karne ya 21. Mwanga wa Lugha, 7(1), 77-88.
dc.identifier.urihttps://ir-library.kabianga.ac.ke/handle/123456789/1201
dc.language.isoother
dc.publisherMwanga wa Lugha
dc.subjectArdhi
dc.subjectUtandawazi.
dc.titleChangamoto Zinazokabili Umiliki na Matumizi ya Ardhi Barani Afrika: Udurusu wa Riwaya Tatu za Karne ya 21
dc.typeArticle

Files

Original bundle

Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Jarida+la+Mwanga_7(1)-77-88.pdf
Size:
283.96 KB
Format:
Adobe Portable Document Format

License bundle

Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: