Ni Mvit̪a ni Mvita?: Uchanganuzi wa Usuli wa Toponimi za Mitʰaa ya Mambasa, Kenya

Loading...
Thumbnail Image

Date

Journal Title

Journal ISSN

Volume Title

Publisher

East African Journal of Swahili Studies

Abstract

Miji yot̪ʰe ulimwenguni imepawa majina ili kuitambulisha. Majina haya ni hazina ya mapisi na ut̪amad̪uni kuwahusu wakaaji wa miji hiyo. Namna inavoitwa, fasiri na fasili za majina hayo husema mengi kuhusu maana na nyusuli zake. Makala haya yamechunguza toponimi ya baadhi ya mitʰaa ya mji wa Mambasa, Kenya. Madhumuni yalikuwa ni kuchanganuwa nyusuli za majina kwa kubainisha t̪afaut̪i za kimat̪amshi ya majina hayo, kuthibit̪isha kuwa t̪afaut̪i hizi zaleta t̪afaut̪i ya maana ya majina, na kwamba toponimi za mitʰaa hiyo imeelemeya kwelezeya maumbile ya mazingira ya mahali hapo jambo linaloshuhud̪iwa katika jamii nyengine za Kibantu, Kenya. Tulitumiya T̪arat̪ibu za Ulinganisho na Toponimi Kina ili kuchanganuliya data yetu. Data yetu tuliipata kwa kuwauliza wazee wa miyaka 50 na zaidi ambao wana maelezo simulizi kuhusu fasili za majina hayo na data ya upili. Kwa kulinganisha na lugha za jamii zinazokaribiyana za Kimvit̪a, Kimijikenra, Kipokomo na lugha za Kibantu kut̪oka bara Kenya tuliweza kung’amuwa kuwa majina haya ya Mambasa yanashabihiyana na yale ya lugha nyengine hivo kutupa ufunuwo mpya kuhusu maana za majina hayo. Tumepata kuwa ut̪amkaji wa majina unaleta t̪afaut̪i ya maana na hivo usuli wao piya ni t̪afaut̪i na ilivozoweleka. Tumepata kuwa majina ya kale yaliitwa kutegemeya maumbile ya mazingira na majina ya mitʰaa ya kisasa yameelemeya zaidi vitu au majengo yaliyoko hapo. Kupitiya makala haya tunaamini tumet̪owa fasili mpya kuhusu mitʰaa hii na hivo kuwapa fikira nyengine wataalamu wa Chimbo, Ut̪alii na Isimu kuhusu majina haya na historiya inayobebwa na majina haya.

Description

Jarida la Uchanganuzi wa Usuli wa Toponimi za Mitʰaa ya Mambasa, Kenya

Citation

Karama, M. (2021). Ni Mvit̪a ni Mvita?: Uchanganuzi wa Usuli wa Toponimi za Mitʰaa ya Mambasa, Kenya. Jarida la Afrika Mashariki la Masomo ya Kiswahili, 3(1), 78-90.

Endorsement

Review

Supplemented By

Referenced By